Sera za Dkt. Samia zawagusa wajasiriamali Uvinza

0

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi kwa akina mama wajasiramali wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, ambao wamekuwa wakipata changamoto ya kukosa eneo maalum na sahihi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Alisema, Serikali kwa kushirikiana na wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Kigoma watajengea mabanda maalum ya kisasa wanawake hao ili wafanye shughuli zao kwa hali salama na kukuza soko lao kwa kuuza bidhaa zao mahali pazuri.

Rais Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo iliyowagusa maelfu ya wanawake wa Uvinza, leo Septemba 13, 2025 wakati akizungumza na wananchi wilaya hiyo katika muendelezo wa mikutano yake ya kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Tambuka reli.

Akizungumzia suala la upatikanaji wa dawa katika hospitali na vituo vya afya, Rais Dkt. Samia amesema serikali yake inayotokana ba CCM imefanikiwa kuongeza asilimia 11 ya upatikanaji wa dawa na kupelekea kufikia asilimia 91, hata hivyo alisema bado serikali itajenga kituo cha afya kipya katika Kata ya Kazuramimba.

Aidha, akizungumzia uboreshaji na utoaji wa huduma bora katika sekta ya Elimu, Rais Dkt. Samia alisema zaidi ya Bilioni 13 zumetumika katika elimu ya msingi ambapo shule mpya 34 zimejengwa, Bilioni 19 zimetumika katika Elimu ya sekondari na kufanya idadi ya shule za sekondari kufikia 31.

Katika juhudi za serikali kuwagusa Vijana, Bilioni 2.8 zimetumika katika ujenzi wa chuo cha VETA ili kuwaongezea ujuzi vijana na uwezo wa kujiajiri.

Vilevile, Rais Dkt. Samia amesema iwapo atapewa ridhaa, serikali yake itaendelea kuleta mbolea na pembejeo ya ruzuku kwa wakulima na wafugaji ndani ya wilaya ya Uvinza na mkoa wote wa Kigoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here