MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema moja kati ya jambo ambalo aliambiwa ni changamoto kwa wakazi wa wilaya ya Manyoni, kukosa usikivu mzuri wa matangazo ya moja kwa moja kutoka TBC.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Manyoni, mkoani Singida, Septemba 9, 2025, Rais Dkt. Samia amewaeleza wakazi wa Manyoni kuwa, Serikali inashughulikia jambo hilo kupitia mradi wa unaosimamiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Vilevile, ameeleza kuwa Serikaili itajenga kituo cha kurushia matangazo cha redio masafa ya FM katika mji wa Itigi ili TBC iweze kusikika vizuri.
Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuwapa fursa wananchi wa Singida kusikia taarifa za Taifa lao kutoka katika kituo chenye uhakika zaidi.