Na Mwandishi Wetu
KUKAMILIKA kwa bandari jumuishi ya Mangapwani kunatarajiwa kupunguza gharama za kushusha mizigo bandari ya Mombasa kisha kuletwa Zanzibar au Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari eneo la mradi, Mhandisi Salum Udi Ussi wa Wizara ya Ujenzi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), alisema kukamilika kwa bandari hiyo itakayogharimu Dola za Kimarekani Milioni 300.
Alisema, bandari hiyo inatarajiwa kuwa kitovu cha bandari kwa nchi za Afrika Mashariki.

“Bandari itakuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa ambazo zilikuwa zinashushia mizigo bandari ya Mombasa.”
Meneja wa Msaidizi wa Mamlaka ya Mafuta na Gesi Zanzibar (ZURA), Joseph Mwambalanga alisema, mita kwa ajili ya kushushia mafuta zimeshafungwa.
“Flow meter zimeshafungwa katika sehemu za kushushia mafuta” alisema.
Alibainisha kuwa, sambamba na mradi huo utakaochukua miaka mitatu, pia kutajengwa tenki kubwa la mafuta ambalo litatumiwa na wafanyabiashara na serikali.