Rais Mwinyi: SMZ itaendelea kuwekeza kwenye michezo

0

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), itaendelea kuwekeza zaidi katika michezo kwa kuendelea kujenga viwanja vipya vya michezo vya kisasa.

Akizungumza na viongozi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA), Ikulu Zanzibar leo 18 Juni, 2025, walipoenda kujitambulisha kuwa Serikali imeamua kufanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kukuza uchumi, fursa za ajira na kuimarisha afya.

Rais Dkt. Mwinyi pia aliwapongeza BAMATA kwa kuandaa michuano hiyo kila mwaka na ametaka mwaka huu kufanyikia Zanzibar kwani kuna viwanja vya kisasa na vya kutosha kwa michezo yote.

“Pia itakuwa fursa ya kuvitangaza viwanja vyetu Kitaifa” alisema na kuongeza kuwa pia itadhihirisha uhusiano wa karibu wa vikosi vya ulinzi na usalama na Serikali ya Mapinduzi (SMZ).

Mwenyekiti wa baraza hilo, Brigedia Jenerali Said Khamis alisema wameridhia michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 14 mwaka huu, kufanyika Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here