Waziri Ridhiwani aipongeza LESCO kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi

0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amepongeza Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO) kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake.

Ridhiwani ametoa pongezi hizo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo wanaomaliza muda wao.

“Nitumie fursa hii kuwapongeza kwa moyo wa dhati kwa kutekeleza vema majukumu yenu kwa ufanisi ili kuhakikisha malengo ya kuanzishwa LESCO yanatimia,” alisema.

Aidha, alisema katika kipindi cha miaka mitatu, LESCO imefanya kazi nzuri ya kuishauri Serikali kuhusu sera zinazohusu masuala ya Ajira na Kazi; upangaji wa kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi; Uridhiaji wa mikataba ya Shirika la Kazi Duniani; na ushirikishwaji wa wadau wa Utatu (Serikali, Waajiri na Wafanyakazi) katika masuala ya kazi, Uchumi na jamii.

Alitoa rai kwa wajumbe wa baraza hilo kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuhakikisha sekta ya kazi na ajira inazingatia misingi ya kazi zenye staha kwa maslahi ya wafanyakazi na waajiri.

Awali, Mwenyekiti wa LESCO Dkt. Samwel Nyantahe ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano katikia kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao.

Uongozi wa Baraza hilo unamaliza muda wake Septemba 12, 2024 na kwasasa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza mchakato wa kuwapata wajumbe wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here