MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unaendelea kuwapatia wananchi elimu na uhamasishaji kuhusu shughuli zake kupitia banda lake katika Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Kupitia ushiriki wake katika maonesho haya, UCSAF inalenga kuwajulisha wananchi kuhusu mchango wake katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wakazi wa maeneo ya vijijini pamoja na maeneo ambayo hayavutii wawekezaji wa kibiashara, ili kuimarisha usawa wa mawasiliano nchini.
