Wananchi wa vijijini wanufaika na elimu kuhusu ruzuku ya ujenzi wa minara

0

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeendelea kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo ya vijijini waliofikiwa na huduma za mawasiliano kupitia minara 758 inayojengwa kwa ruzuku ya Serikali. Ujenzi wa minara hii unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini na umefikia asilimia 78.63 ya utekelezaji wake.

Kampeni hii inalenga kuwafahamisha wananchi kuwa, ujenzi wa minara ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini unatekelezwa kwa ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia UCSAF.

Ruzuku hii inalenga kuhakikisha wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa wawekezaji wa sekta binafsi, wanapata huduma za mawasiliano bila kuathiriwa na changamoto za kijiografia au umbali wa maeneo yao.

Wananchi waliopatiwa elimu hii wamesema, huduma za mawasiliano zimeleta mabadiliko katika maisha yao ya kila siku, hasa katika nyanja za kijamii, kiuchumi, na kielimu.

Aidha, wamepongeza juhudi za UCSAF kwa kuwaelimisha kuhusu mchango wa Serikali katika kuwafikishia huduma hizi, jambo ambalo limeongeza uelewa wao na ushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here