KAMPENI ya elimu kwa umma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeendelea kufanyika katika Kijiji cha Mwanzoya, Kata ya Itubukilo, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Kupitia kampeni hiyo, wananchi wamepatiwa elimu kuhusu dhima na majukumu ya UCSAF katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano hususan maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.
Aidha, wananchi wamehamasishwa kutumia fursa za mawasiliano kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu ya mawasiliano iliyojengwa katika maeneo yao.
Kampeni hii ni sehemu ya juhudi za UCSAF kuhakikisha jamii inapata uelewa sahihi kuhusu miradi inayotekelezwa na manufaa yake, sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya Mfuko na wananchi.