Wanachama 453 wa ACT wajiunga CCM

0

WANACHAMA 453 kutoka ngome ya ACT Wazalendo kisiwani Pemba leo wamejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kiongozi wao, Faki Ali Juma, amesema uongozi bora wa Serikali ya Awamu ya Nane umewavutia na wakaahidi kumuunga mkono kwa kishindo Mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ifikapo Oktoba 29, 2025.

Wanachama hao wapya waliapa Kiapo cha Utii kwa Chama Cha Mapinduzi katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni za CCM, Pemba iliyofanyika Uwanja wa Gombani ya Kale, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba Septemba 15, 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here