MBUNGE wa Kibaha vijijini Michael Mwakamo amewataka walimu wote wa shule za Kibaha kushirikiana pamoja na wazazi ili kuendelea kuimairisha ufaulu wa wanafunzi wa Kibaha vijijini.
Alitoa wito huo kwenye hafla ya kuwapongeza walimu wa kidato cha tano na cha sita kwa shule za halmashauri ya wilaya ya Kibaha zilizofanyika Machi 5, 2025, katika shule ya sekondari Ruvu girls.
Mwakamo alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha Regina Bieda kwa kuandaa hafla hiyo ya kuwapongeza walimu kwa kuleta matokeo mazuri, kwa kidato cha tano na cha sita, kwani italeta chachu na hamasa ya walimu kufanya kazi kwa bidii.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Regina Bieda alitoa pongezi kwa Shule zilizoongoza kwa matokeo mazuri na kutaka Shule hizo ziwe mfano wa kuigwa kwa Shule nyingine.
Shule hizo ni pamoja na Shule ya sekondari Heritage, Shule ya sekondari Kilangalanga, Ruvu girls na nyinginezo.

Mmoja wa walimu walio shiriki kwenye hafla hiyo Kamila Pokela amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, kwa niaba ya walimu wote kwa kutambua thamani ya walimu kwa kuandaa halfa hiyo ya kutoa pongezi kwa walimu kwa kazi nzuri waliyo ifanya.
Hafla hiyo ilihitimishwa na Bieda kwa kuwakumbusha walimu na watumishi wote wa Kibaha kushiriki katika Mwenge wa Uhuru Aprili 9, 2025.
