Ukabila usipewe nafasi, tujenge Taifa – Kinana

0
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amewasisitiza wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuachana na tabia za ukabila akieleza kuwa ni mambo ya kizamani na yanawagawa.

Akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, Kinana Aprili 15, 2024 mjini Shirati wilani Rorya alisema, nchi kuwa na makabila ni jambo la kawaida ila ukabila ni jambo baya, lisilopaswa kupewa nafasi.

Kinana alisema hayo baada ya baadhi ya wajumbe kuibua hoja kwamba kuna mambo yanafanyika katika wilaya ya Roria ambayo yanaashiria kuwepo kwa changamoto ya ukabila miongoni mwao.

Alieleza kwamba, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ametoka mkoani humo, kutoka kabila dogo, lakini ameongoza nchi kwa miaka 24, na kwamba alipendwa, aliheshimiwa na kuthaminiwa.

“Sasa usimpe mtu nafasi ya uongozi kwa sababu ya kabila lake, dini au umbile usimuhukumu, hayo ni mambo ya kizamani sana, tuangalie mtu anauwezo atafanya kazi atajituma na kujitolea, mnampima kwa vigezo sio kwamba huyu ni ndugu yangu.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here