Ujenzi wa Jengo la Shule ya Uchumi UDSM wafikia asilimia 94

0

MRADI wa ujenzi wa Jengo la Shule ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaendelea kwa mafanikio makubwa.

Mradi huu muhimu ulianza Julai 9, 2021 na ulitarajiwa kukamilika ifikapo 30 Juni 2025, kwa kipindi cha miezi 18 ya ujenzi.

Hadi sasa, hatua ya utekelezaji imefikia asilimia 93%, ishara kwamba jengo linaelekea kukamilika kwa wakati. Jengo hili linalojengwa kwa ubora wa kisasa litatoa nafasi bora za kusomea, kufundishia na kufanya tafiti, hivyo kuongeza hadhi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama kitovu cha elimu ya juu na utafiti barani Afrika.

Mradi huu ni kielelezo cha uwekezaji madhubuti katika elimu ya juu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here