UCSAF yatoa elimu kwa wananchi wa Msolokelo kuhusu maboresho ya mawasiliano

0

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umetoa elimu kwa wananchi wa Kijiji cha Msolokelo, Kata ya Pemba, wilayani Mvomero mkoani Morogoro kuhusu maboresho ya huduma za mawasiliano yanayofanywa na Serikali ili kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini wanapata mawasiliano ya uhakika.

Elimu hiyo imetolewa na maafisa wa UCSAF kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya simu ya Vodacom kupitia ruzuku ya Serikali inayotolewa na UCSAF.

Lengo la elimu hiyo ni kuwajengea wananchi uelewa juu ya manufaa ya mradi huo, matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano, na nafasi ya teknolojia katika kuboresha maisha yao.

Wananchi walioshiriki mafunzo wamepongeza hatua hiyo huku wakieleza kuwa imewasaidia kuelewa namna bora ya kutumia huduma hizo, katika kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yao.

UCSAF inaendelea kutoa elimu kwa vijiji vingine vilivyonufaika na miradi ya maboresho ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma hizo zinawanufaisha wananchi kikamilifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here