‘Tuwekeze kwenye maendeleo ya rasilimali watu’

0

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhwan Jakaya Kikwete amesema, kuna haja ya kuimarisha uhusiano wa wa muda mrefu kati ya Tanzania na Japan.

Kikwete alitoa kauli hiyo Agosti 27, 2025, Dar es Salaam wakati wa ziara ya Gembรก Koichiro, Makamu Spika wa Baraza la Wawakilishi la Japan, na ujumbe wake.

Alisema, kuna umuhimu wa kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu, hasa vijana na kusisitiza, Tanzania imeendelea kuwa na ukuaji thabiti wa uchumi, lakini ili kufungua kikamilifu uwezo wake, ni lazima kuwa na kipaumbele katika maendeleo ya rasilimali watu.

Alisema, kuwekeza kwa vijana katika ujuzi, maarifa, na ustawi wao ni uwekezaji mkakati wa kwanza kwa mustakabali wa Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here