TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imekutana na Wataalam wa Ustawi wa Jamii na Saikolojia.
Kaimu mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, ameeleza kuwa lengo la kukutana na wataalamu hao ni kufahamu madhara ya kisaikolojia na kijamii yaliyotokana na matukio ya wakati na baada ya uchaguzi Mkuu.
Mkutano huo wa Tume na Wataalamu hao umefanyika katika Ukumbi wa Ngorongoro uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa na Wataalamu hao kutoka taasisi za kiserikali na za kiraia ni pamoja na namna ya kuyashughulikia madhara hayo.