WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameiaga na kuikabidhi bendera ya Taifa timu ya mpira wa kikapu ya Dar City ikiwa ni ishara ya kuwatakia mafanikio katika ligi ya mchezo wa kikapu Afrika (Basketball Africa League) (BAL) inayotarajiwa kuanza Machi 27, 2026 Pretoria Afrika Kusini.
Tukio hilo limefanyika Machi 23, 2026 jijini Dar es Salaam, wakati timu hiyo ikiwa tayari kwa safari ya Afrika Kusini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayoshirikisha vilabu bora kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.
Makonda amewataka wachezaji hao kuzingatia nidhamu, mshikamano na uzalendo ili kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Kwa upande wao, wachezaji wa Dar City wameahidi kupambana kwa juhudi zote kuhakikisha wanaleta matokeo chanya na kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano hayo ya kimataifa