Teknolojia ya akili mnemba kutumika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

0

TANZANIA imeandaa kwa mara ya kwanza Mkutano wa Kimataifa unaojadili matumizi ya teknolojia ya Akili mnemba (AI) katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam Oktoba 8 ,2025 Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Peter Msoffe amesema teknolojia ya akili mnemba inatoa fursa ya kutabiri athari za mabadiliko ya tabianchi, kusaidia juhudi za usafi wa mazingira na kuhifadhi bioanuai.

Mkutano huo umeratibiwa na Kamati ya Wataalamu ya Teknolojia ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) ambapo Tanzania ni Mwanachama wa UNFCCC na Ofisi ya Makamu wa Rais ni kiungo wa mkataba huo.

“Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa ni upatikanaji wa fedha kwa miradi ya akili mnemba inayolenga mabadiliko ya tabianchi, mafunzo na ujenzi wa uwezo kwa wataalamu wa nchi zinazoendelea na maendeleo ya miundombinu ya teknolojia na uchambuzi wa data kwa kutumia AI.

Prof. Msoffe amesema mkutano huo ni fursa muhimu kwa vijana, wataalamu na taasisi za Tanzania kujifunza, kushirikiana na kunufaika na teknolojia ya AI katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

“Mkutano huo unawakutanisha zaidi ya washiriki 200 kutoka nchi mbalimbali duniani, ukiwa na lengo la kuhimiza matumizi ya teknolojia za kisasa katika kulinda mazingira, hasa kwa nchi zinazoendelea.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here