TCB yadhamiria kuwawezesha wakandarasi nchini

0
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo.

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) ipo mbioni kuanza mpango wa kuwawezesha wakandarasi wanaotekeleza miradi inayosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), miradi ya umeme na maji ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa kwa mujibu wa mikataba yao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TCB Adam Mihayo alisema hayo jijini Dar es Salaam kwenye Mkutano na wahariri na waandishi wa habari wenye lengo la kuelezea mafanikio ya benki hiyo ambayo awali ilijulikana kama Benki ya Posta Tanzania (TPB).

Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Regina Semakafu, akifafanua jambo wa kikao kazi cha Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na Wahariri wa Vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR). Picha zote na Francis Dande, Habari Mseto Blog.

Mihayo alisema, wapo kwenye mazungumzo na uongozi wa TARURA ili waanze utaratibu huo katika kuchochea maendeleo ya nchi.

Alisema, benki hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwenye miradi mikubwa mbalimbali ukiwemo wa Treni ya Kisasa (SGR), ambapo wamekuwa na uhusiano mzuri na Shirika la Reli Tanzania (TRC) na wao ndio waliosaidia uagizaji wa mabehewa ya treni hiyo.

Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akizungumza katika mkutano huo.

“Hata wakandarasi wakubwa kabisa wa mradi huo ni wateja wetu, na sio hivyo tu, hata wale sub-contractors tumekuwa tukiwasapoti, sasa kupitia sapoti hiyo, tunataka kuhamia sehemu nyingine, kwasasa tupo kwenye maongezi na TARURA kuhakikisha wale wakandarasi, tunawawezesha kimtaji, kwa kufanya hivyo tunaamini watamaliza miradi yao mapema na Serikali itafikia lengo lake,” alisema.

Mihayo alisema, mbali na wakandarasi wa barabara, wanatarajia kuwezesha miradi ya maji na umeme, kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameshiriki kwa kiasi kikubwa kusukuma ajenda muhimu za Serikali na kuchangia ukuaji wa uchumi.

Mkurugenzi wa Masoko Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Deo Kwiyuka, akizungumza wakati wa kikao kazi cha Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR).

“Pia tumetenga Shilingi Bilioni 300 kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanachangia asilimia 30% ya ukuaji wa uchumi wa nchi,” alisema na kuongeza kuwa, kwa kufanya hivyo watakuwa na mtaji wa kutosha, hivyo wataongeza ajira na kuchangia ongezeko la kodi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here