Tanzania na Msumbiji kuanzisha Jukwaa la wafanyabiashara

0

Na Mwandishi Wetu

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji Phaustine Kasike, amekutana na Silvino Augusto José Moreno, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Msumbiji kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Jijini Maputo, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali ili kufanikisha ushirikiano katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji.

Vilevile, Viongozi hao wamekubaliana kutafuta mbinu na mikakati mahsusi ya kuongeza kiwango cha biashara baina nchi hizi ili kiende sambamba na uhusiano wa kindugu, kihistoria na kijiografia baina ya nchi hizi.

Moja ya maeneo yaliyopendekezwa ni kuanzisha Jukwaa la Pamoja la Biashara litakalowakutanisha Wafanyabiashara na wadau wengine muhimu ili kubadilishana uzoefu, kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi na kubaini namna ya kunufaika nazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here