TANAPA yaendelea kutambulika Kimataifa katika ubora wa huduma

0

NAIBU Kamishna wa Uhifadhi, Massana J. Mwishawa, anayeshughulikia Maendeleo ya Biashara TANAPA, amepokea Cheti cha ISO 9001:2015 kwa niaba ya Kamishna Mussa Nassoro Kuji, katika hafla ya iliyofanyika Januari 24, 2025 yalipo Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jijini Arusha.

Cheti hicho kilikabidhiwa kwa TANAPA na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambaye ni Dkt. Ashura Katunzi, kwa kutambua jitihada za TANAPA katika kutoa huduma kwa viwango vya kimataifa na kuimarisha huduma bora kwa wageni na wadau wanaotembelea hifadhi hizo.


Hifadhi zilizopata cheti hicho ni pamoja na Ofisi ya Makao Makuu ya Shirika, Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Hifadhi za Taifa Kilimanjaro, Arusha, Mkomazi, Manyara na Tarangire.

Utoaji wa huduma bora kwa wageni umechochea ongezeko la watalii na mapato katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Mafanikio haya pia ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya utalii pamoja na kutangaza utalii hasa kupitia filamu ya “Tanzania The Royal Tour” iliyoleta mafanikio makubwa sana nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here