NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, ameikabidhi Taifa Stars kiasi cha Shilingi Milioni 10 za goli la mama.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa kiasi cha Shilingi Milioni 20 pamoja na mdau wa michezo, Azim Dewji, ambaye ameahidi kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa timu hiyo.
Stars imejinyakulia fedha hizo baada ya ushindi wa goli 1 – 0, dhidi ya Mauritania, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Agosti 06, 2025.