‘Suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira linamuhusu kila mtu’

0

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema, suala la Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira unamuhusu kila mtu sababu unagusa maisha ya kila siku ya binadamu.

Akiongea katika kikao kazi baina yake na viongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kilichofanyika Dodoma, Juni 25, 2025 alisema kuharibu Mazingira ni kuharibu maisha ya viumbe hai.

Katika kikao hicho Waziri Masauni ameupongeza uongozi wa NEMC kwa namna ambavyo wanafanya kazi katika Uhifadhi na Utunzaji mazingira huku akieleza juhudi zaidi inapaswa katika utoaji wa elimu.

Alisema, pamoja na changamoto ambazo wanapitia lakini baraza linajukumu kubwa la kuhakikisha jamii inapata elimu katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira kupitia wataalamu ambao wapo katika ofisi hizo.

“Niwapongeze kwa namna mnavyoshirikiana katika kutekeleza majukumu yenu ambayo mmekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa safi na salama,”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware alisema, suala la elimu ndio jambo ambalo wamekuwa wakilitazama zaidi ili kuifanya jamii inakuwa na uelewa kuhusu mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here