STAMICO na Buckreef Gold watoa elimu ya uchimbaji wa madini na umuhimu wake

0

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Kampuni ya dhahabu ya Buckreef Gold wametoa elimu kuhusu uchimbaji wa madini na umuhimu wake katika jamii kwa wananchi waliotembelea
migodi hiyo.

Elimu hiyo imetolewa wakati wa ziara ya washiriki wa maonesho ya tano ya madini waliokwenda kutembelea migodi hiyo miwili na kujionea jinsi inavyotoa fursa kwa vijana wa Tanzania iliyoandaliwa na waandaji wa Maonesho ya Tano ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Akitoa elimu ya uchimbaji mdogo Msimamizi wa Kituo cha Mfano cha wachimbaji wadogo, Mhandisi migodi Victor Olal alisema, STAMICO inafanya na kusimamia shughuli za uchimbaji madini sambamba na kuendesha mafunzo ya uchimbaji kwa vitendo ili kuhakikisha wachimbaji wadogo wanafanya uchimbaji wenye tija na manufaa.

Alisema, kupitia vituo hivyo STAMICO imeweza kuwafanya wachimbaji kuelewa umuhimu na kutumia teknolojia ya kisasa katika uchimbaji hivyo kupelekea baadhi ya wachimbaji wadogo kuwa na shauku ya kutumia tekinolojia hiyo katika maeneo yao.

“Ni jambo la kujivunia kuona wachimbaji wadogo wengi wameanza kuelewa na kuthubutu kutumia tekinolojia hii, kwani hadi sasa baadhi ya wachimbaji wameanza kujenga mitambo ya uchenjuaji inayofanana na hii,” aliongeza Olal.

Alisema, kupitia sekta ya uchimbaji mdogo vijana wengi wanapata fursa ya ajira, kujifunza uchimbaji wa kisasa, biashara hata kujipatia maendeleo binafsi.

“Vituo hivi hutoa ajira kwa watu wengi wazawa, vinatumia teknolojia ya kisasa hivyo kupunguza athari zinazotokana na kemikali hatarishi kama zebaki”

Ziara hii pia imetoa fursa kwa washiriki kutembelea shughuli za uchimbaji mkubwa na kujionea jinsi dhahabu inavyopatika kuanzia hatua za utafiti, uchimbaji na uchakataji wake katika mgodi wa Buckreef Gold

Aidha, wameweza kuona manufaa ya mgodi huu kwa watanzania yakiwemo ajira, uwajibikaji katika huduma za kijamii zikiwemo,hospitali, shule na miundombinu ya barabara.

Mhandisi Mwandamizi wa Migodi Erick Yohana amefafanua kuwa kampuni ya Buckreef inafanya kazi kwa weledi katika kila kada na kuendeshwa kwa 100% ya waajiriwa watanzania.

Alisema, kampuni hiyo inazidi kujiongezea uwezo wa uzalishaji jambo litakalopelekea kuongezeka kwa fursa za ajira kwa Watanzania.

Vilevile Mgodi wa Buckreef unafanya kazi na wazabuni na wakandarasi wa Kitanzania katika kupata bidhaa na huduma.

Aliongeza kuwa, shughuli za uchimbaji mgodini hapo huzingatia sana suala la usalama wa watu, vifaa, na vyote vinavyozunguka mgodi huo.

Kutembelea migodi hiyo miwili kumewawezesha washiriki hao kutofautisha aina za uchimbaji yaani uchimbaji mkubwa na uchimbaji mdogo na kujionea umuhimu wa kila mmoja katika jamii na Serikali kwa ujumla

Akiongea moja washiriki katika ziara hiyo Kelvin Haule ametoa pongezi kwa STAMICO pamoja na Buckreef kwa kutoa fursa kwa watanzania ya kusimamia shughuli za uchimbaji katika migodi hiyo na kutoa nafasi kwa wageni mbalimbali kujionea na kujifunza.

Aidha, ametoa pongezi kwa Kamati ya kuratibu Maonesho ya Tano ya Madini kwa kuandaa ziara katika migodi mbalimbali ili kuangalia sekta ya madini inavyotoa fursa za ajila na Maendeleo kwa jamii ya wa watanzania.

Washiriki wa maonesho ya Madini wametembelea katika Mgodi wa Buckreef na kituo cha mfano cha wachimbaji wadogo chenye mgodi na mtambo wa kuchakata dhahabu ili kujionea shughuli mbalimbali za uchimbaji na kuweza kutofautisha aina za uchimbaji madini unaofanyika nchi ikiwemo uchimbaji mkubwa wa kati na uchimbaji mdogo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here