Serikali yaunganisha Shule 1,121 na Mtandao wa Intaneti

0

SERIKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefanikiwa kuunganisha shule za Serikali 1,121 na huduma ya intaneti, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupanua wigo wa matumizi ya intaneti ya kasi (broadband) nchini.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi alisema hayo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka, kuhusu mpango wa Serikali wa kuweka huduma ya bure ya intaneti kwenye shule na vyuo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here