Serikali yatenga zaidi ya Bilioni 50 kukarabati barabara za TARURA

0

ZAIDI ya Shilingi Bilioni 21 zimetengwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya dharura kuhudumia kukarabati barabara za TARURA zilizoharibika nchini.

Hayo yamesemwa Bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Zainab Katimba kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la Shabani Omari Shekilindi, mbunge wa Jimbo la Lushoto aliyetaka kujua hatua za dharura za Serikali zilizochukuliwa kukabiliana na uharibifu wa barabara uliotokea kote nchini.

Akijibu swali hilo Katimba alisema “Serikali imekuwa ikichukua hatua za dharura kurudisha mawasiliano kwenye barabara ambazo zimekatika na imekuwa ikiendelea kuimarisha barabara zetu za wilaya kuhakikisha zinakuwa katika mazingira ambayo zinaweza kupitika katika kipindi cha mwaka mzima.”

Akisisitiza Katimba alisema, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha nyongeza ya bajeti ya dharura ya Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya kuhudumia Barabara zinazoharibika kwa utaratibu wa dharura.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here