Na Sixmund Begashe, Dodoma
SERIKALI inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kujenga vituo vya Askari wa wanyamapori karibu na maeneo ya hifadhi ili kuwa na mwitikio wa haraka wa kukabiliana na wanyapori hao hususan Tembo wanaovamia makazi na mazao ya wananchi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika Bunge la 13, Mkutano Wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akijibu maswali ya Wabunge kwa Waziri Mkuu ambapo amebainisha kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inatekeleza uanzishwaji wa vituo hivyo kwa kila eneo lililokuwa na hatari hizo ili kukabiliana na athari za Wanyamapori hao.
“Sambamba na hilo serikali imekuja na namna mpya ya kuwafukuza Wanyama hao katika baadhi ya maeneo na mojawapo ya mikakati ya Wizara ni yakutumia ndege nyuki (drones) kuwafukuza pindi wanapobainika kuelekea maeneo ya wananchi ” amesema Dkt. Nchemba
Aidha, Dkt. Nchemba ameongeza kuwa Wizara itaendelea kuongeza idadi ya Askari wa wanyamapori katika maeneo yenye upungufu wa Askari ili kukabili kwa haraka na Wanyama hao licha ya kuongeza nguvu katika kukabiliana na ujangili.
Awali Dkt. Nchemba alifafanua kuwa Tanzania ni mwanachama wa mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolinda makundi mbalimbali ya Wanyamapori walioharatibi kutoweka, kutokuwauwa au kutosafirishwa kwa mazao yake wakiwemo Tembo