Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Hanang kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Katesh Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Rais Samia alifika Katesh kwa ajili ya kuwapa pole wananchi wa maeneo hayo ambao wameathirika na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni.





