Na Florid Mapunda, Dar es Salaam
SEKTA ya bandari nchini imekua mojawapo ya vyanzo vikuu vya mapato na kupelekea kukuza uchumi wa nchi na wananchi wake ambao wamepata ujira wa moja kwa moja ama usio wa moja kwa moja.
Nchi yetu imebarikiwa kuwa na Pwani ndefu kutoka Kaskazini ya Tanga mpaka kusini mwa Mtwara ambako inapakana na pwani ya Msumbiji, pwani hiyo yote ina urefu wa kilomita 1424 na kuna bandari za kutosha, baadhi yake ni bandari ya Tanga, Dar es Salaam, Bagamoyo na Mtwara. Hizo zote hutumika kwa ajili ya kuingiza na kutoa mizigo hapa nchini.
Pwani hizi zimekuwa zikitumika tangu enzi za utawala wa Waarabu, Wajerumani na Waingereza na kupelekea baada ya uhuru wa Tanganyika kufanyiwa maboresho na kujengwa upya kwa lengo la kusafirishia bidhaa za kuingia na kutoka nchini.
Bandari hizo zimekuwa na tija kwa Tanzania na hata kwa nchi zote zinazotuzunguka kwani hutumia kwa ajili ya kusafirisha bidhaa zao kwenda na kutoka Ughaibuni. Nchi hizo ni Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na Zimbabwe.
Nchi nyingine zinazojinufaisha kwa kutumia bandari zetu ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia, na Zimbabwe.
Makala hii inaelezea kwa kina namna gani nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inavyofaidika kupitia bandari za Tanzania hususani bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo za ziwa Tanganyika katika kusafirisha shehena zake mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa mapema juma hili alipotembelea bandari ya Dar es Salaam inasema kuwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaongoza kwa kuagiza shehena nyingi zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine zinazotuzunguka.
“Nchi ya DRC pekee katika mwaka wa 2024/2025 imepitisha shuhena kwenye bandari zetu yenye zaidi ya tani milioni 5.9, ni kiasi kikubwa ambacho haijawahi kutokea na hiyo yote ni kutokana na kuboresha miundombinu yetu mbalimbali ya ndani na nje ya bandari”, alisema Msigwa.
Kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan cha kuboresha mahusiano ya nchi yetu na nchi za jirani hususani nchi ya Kongo na kutenga eneo maalumu lenye ukubwa wa hekta 45 katika bandari kavu ya Kwala kwa ajili ya ili liwe eneo lao la kuhifadhi shehena zao.
Hiyo imeongeza ari kwa wafanyabiashara kuendelea kutumia bandari za Tanzania kwani wanaona usalama wa bidhaa zao ni mkubwa hivi sasa ikilinganisha na nchi nyingine zenye bahari.
Mnamo Machi 19,2025 uongozi kutoka nchini Kongo na Burundi walitembelea bandari Kavu ya Kwala na kujionea miundombinu jinsi ilivyoboreshwa, wakaridhika na kusema sasa malalamiko ya afanyabiashara kutoka nchini Kongo na Burundi hayatakuwepo tena kwani mazingira yote ya ufanyaji kazi wake yameboreshwa kwa kiasi kikubwa tangu ndani mpaka nje.
Ujumbe huo ulingozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi kutoka nchini Burundi Christine Niragira na Mwakilishi wa Wizara ya Uchukuzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) Roger Te- Biasu.
“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania na tunampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri inayofanyika hapa Kwala na kwa kutupatia eneo hili kwani ni njia ya kurahisisha ufanyaji biashara kati ya Tanzania na Burundi nasi kwa sasa tunaendelea kuliendeleza eneo hili haraka”, Alizungumza mmojawapo wa viongozi kutoka nchini Kongo.
Kwa nini Kongo wameichagua Tanzania?
Serikali na wafanyabiashara wa Kongo wamevutiwa kuitumia bandari ya Dar es Salaam kwa kupitisha mizigo yao kutoka nje ya nchi lakini pia kusafirisha shehena zao kwenda ughaibuni kupitia bandari hiyo kutokana ubora wa miundombinu ya barabara na ukaribu kati ya Kongo na Tanzania.
Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ni rafiki kwa nchi ya kongo kwa sababu ya umbali, ambapo kutoka DRC mpaka Dar es Salaam ni kilomita 3753, wakati kutoka Kongo mpaka Mombasa nchini Kenya ni zaidi ya kilomita elfu tano.
Hivyo basi Serikali ya Kongo pamoja na wafanyabiashara wanapenda kutumia bandari yetu kutokana na sababu ya umbali huo.
Taarifa zilizochapishwa na mtandao wa google zinasema kwamba gharama nafuu za uchukuzi wa shehena katika bandari ya hiyo ni mojawapo ya sababu inayo