REA yapongezwa kwa utekelezaji wa ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia

0

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema amevutiwa na teknolojia ya majiko banifu yanayotumia umeme na gesi kwa ajili ya kupikia.

Alisema hayo alipotembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini Dodoma, ambapo alisema amevutiwa na teknolojia hiyo kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha Wananchi wengi wanahamasika na kuanza matumizi ya teknolojia za nishati safi ya kupikia vijijini na mijini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (DRE); Mhandisi, Jones Olotu alisema katika maonesho hayo wamealika Wadau wa teknolojia ya majiko banifu ambayo ni salama kwa mazingira na kwa afya za Watumiaji.

Alisema, majiko hayo yamekuwa yakiuzwa kati ya Shilingi Milioni 3 hadi Milioni 1.5 na kwamba yameanza kutumiwa na Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Akizungumzia usambazaji umeme kwenye vijiji na vitongoji; Mhandisi Olotu alisema idadi ya vijiji vilivyofikiwa hadi na nishati ya umeme ni vijiji 12,031 kati ya vijiji 12,318 sawa na asilimia 97.7 na kwa upande wa vitongoji. Tanzania ina vitongoji 64,359, vyenye umeme ni 32,827 na visivyo na umeme ni 31,532.

Katika hotuba yake wakati wa kufunga rasmi maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma; Waziri Mkuu ameitaka REA kuendelea kushirikiana na Sekta Binafsi ili kuhaongeza wigo wa Taasisi za Umma katika matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Taasisi zinazotumia nishati ya kuni na mkaa kupikia kwa zaidi ya Watu 100.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here