RC Makalla apiga marufuku biashara kwenye barabara za Mwendokasi Mbagala

0

. Asema ni Hatari kiusalama, zinasababisha ajali na kukwamisha Mkandarasi kutekeza majukumu

. Ampongeza Rais Dkt. Samia kuridhia kujenga mwendokasi Mbagala – Vikindu Phase 6

. Awataka wananchi kupanda miti Na kuweka bustani katika nyumba zao ili kuifanya DSM ya kijani

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla Leo amefanya Zoezi la usafi Wilaya ya Temeke eneo la Mbagala, ambapo amepiga marufuku ufanyaji Biashara kwenye ujenzi wa Barabara ya mwendokasi na maeneo yaliyokatazwa.

RC Makalla ametumia zoezi hilo kuwakumbusha Wananchi na Viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi Wilaya kuhakikisha wanasimamia usafi Kila jumamos ya mwisho wa mwezi.

Aidha, RC Makalla amewaelekeza Wakurugenzi kusimamia Wakandarasi kuondosha taka kwa wakati na Wakandarasi watakaoonyesha kulegalega wasipatiwe mkataba.

Pamoja na hayo RC Makalla amewapongeza Wananchi kwa mwamko mkubwa wa kufanya usafi jambo lililopelekea Jiji la Dar es Salaam kushika nafasi ya Sita kwa usafi Barani Afrika na kuondosha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, zaidi ya Shilingi Bilioni 3.2 zimetolewa kama mkopo kwa Wafanyabiashara Wanaofanya biashara kwenye Maeneo Rasmi na kutoa wito kwa Wafanyabiashara wengine kuacha kufanya biashara holela.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here