Rais Samia Suluhu Hassan aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Mkoani Dodoma.

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili Msalato, jijini Dodoma katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), pamoja na viongozi wengine wa Serikali akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya (katikati) pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakisilikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma.
Machifu wa Jiji la Dodoma, Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (picha ya chini), pamoja na wananchi wakisilikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakifurahi jambo mara baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, jijini Dodoma. (PICHA NA WUU).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here