Habari Rais Samia awaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni By Ripota Wetu - October 22, 2022 0 FacebookTwitterPinterestWhatsApp Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Boniphace Nalija Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Oktoba 22, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimuapisha Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Wakili Mkuu wa Serikali Dkt.Boniphace Nalija Luhende, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Sarah Duncan Mwaipopo pamoja na Wakuu mbalimbali wa Taasisi wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi wa Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Nalija Luhende pamoja na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Sarah Duncan Mwaipopo mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Nalija Luhende , Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Sarah Duncan Mwaipopo mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam