Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29, 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja Machi 2,2024.



