Rais Mwinyi ashiriki sala ya kumsalia Marehemu Hassan Khamis

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wananchi katika Mazishi ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi Marehemu Hassan Abdalla Khamis aliyefariki jana.

Rais Dkt. Mwinyi alishiriki katika Sala ya Kumsalia Maiti Msikiti wa Al AZHAR Magomeni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Dkt. Mwinyi alifika Nyumbani kwa Marehemu Mpendae Kutoa Mkono wa pole na kuwafariji Wafiwa na kuwataka kuwa na Subira wakati huu wa Msiba huo mzito.

Marehemu Hassan Abdalla Khamis wakati wa Uhai wake aliwahi kufanya Kazi katika Idhaa ya Kiswahili ya Redio Cairo Nchini Misri, Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Abu Dhabi na hadi Mauti yanamfika alikuwa ni Meneja wa Redio ya Kidini ya Kheri FM Jijini Dar es Salaam.

Marehemu amezikwa kijijini kwao Muyuni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here