OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki amesema, Pikipiki zipatazo 916 zitagawiwa kwa Watendaji wa Kata ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Waziri Kairkuki ameyasema hayo wakati alipomuwakilisha Makamu wa Rais katika hafla ya kuufahamisha umma mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Mkoa wa Dodoma.
Akijibu ombi la Mtendaji wa Kata ya Uhuru katika Jiji la Dodoma Christina Mpete kuhusu uwezeshaji wa vyombo vya usafiri hususani ni Pikipiki kwa watendaji hao ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo Kairuki alisema “niwape habari kuwa ombi hilo limekuja wakati muafaka ambako Serikali imeshanunua Pikipiki hizo zitagawiwa wakati wowote kuanzia sasa na tunaenda kwa awamu kwa sasa watendaji 916 watapatiwa Pikipiki hizo.”