‘No reform, no election’ ni mtego kwa jamii yetu

0

Na Mwandishi Wetu

UKIFUATILIA historia ya Mataifa mbalimbali ambayo yameingia kwenye migogoro na vurugu, utagundua siasa imechangia.

Kampeni ya “No Reform, No Election” inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) si jambo la kawaida, bali ina mlengo wa kupenyeza ajenda binafsi.

Historia imetuonyesha kuwa, harakati kama hizi zimeleta madhara makubwa katika Mataifa kama Libya (2011), Sudan Kusini (2013), na Venezuela (2014). Migogoro ya kisiasa iliyoanzishwa kwa madai ya mabadiliko ilisababisha vurugu, kudorora kwa uchumi na mateso kwa wananchi wa kawaida.

Hali kama hiyo ilijitokeza Sudan Kusini, ambapo maandamano na migomo vilitumika kama nyenzo za kuchochea mgawanyiko uliosababisha madhara makubwa. Ni wazi, maandamano na migomo mara nyingi haileti suluhisho, bali huzorotesha hali ya wananchi wa kawaida.

Jamii inataka Umoja, amani na mshikamano, hivyo Chadema kuanzisha vuguvugu lisilo na utaratibu wa kidemokrasia kama “No Reform, No Election” ni sawa na kupanda mbegu ya kusaliti wananchi na pandikizi la uvunjifu wa sheria.

Kwa wale ambao mmeingia kwenye mtego huo, msiache kujiuliza, maendeleo mnayoyataka yatapatikana kwa vurugu na mgawanyiko? Hakuna njia nyingine?

Ajenda zisizoonekana dhahiri ni hatari

Methali ya Kiswahili inasema, “Kikulacho ki nguoni mwako.” Si kila kampeni inayoonekana ina nia njema kwa jamii. Msingi wa demokrasia ni kuheshimu utaratibu wa kisheria na vyombo vya maamuzi vilivyopo.

Wananchi tukumbushane! Tuoneshane mwanga penye giza kuwa kuna mambo mengi yaliyojificha ndani ya kauli mbiu ya “No Reform, No Election” ambayo inaweza kutuvuruga kwenye shughuli zetu za kimaendeleo na mipangilio tuliyozoea katika kupata mikate yetu ya kila siku, muda unaruhusu kuepuka kupigwa mifukoni.

Kampeni hii itufikirishe na tujiulize, inahamasisha maandamano, migomo, na chuki kwa maslahi ya nani?

Mfano wa Wananchi Kukataa Kutumiwa kwa Migomo na Maandamano

Nchini Singapore chini ya uongozi wa Lee Kuan Yew, ambapo tangu miaka ya 1960 wananchi walizingatia maendeleo na nidhamu, walikataa vurugu na maandamano yasiyo na tija. Matokeo yake, Taifa hilo likawa moja ya Mataifa yenye uchumi imara duniani.

Tuendelee kupuuzia miito ya maandamano yasiyoheshimisha, baadhi ya wanaharakati wa kisiasa, wakitambua kuwa suluhu haiji kwa vurumai, migomo, maandamano, matusi, kejeli bali kwa taratibu na mazungumzo watabadilika.

Migomo na maandamano haiwezi kuleta maendeleo, bali huzorotesha uchumi, kuvuruga biashara, na hata kusababisha hasara kwa watu wa kawaida.

Wajibu wetu kama Jamii

Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema, “Uhuru wa mtu mmoja hauwezi kuwa sababu ya kumfanya mwingine asiwe na uhuru wake.”

Wanajamii tunayo nafasi ya kuelewa kuwa, uhuru wa kufanya siasa haupaswi kuvuka mipaka ya taratibu zilizopo ni kuvunja miiko yetu, kwa maendeleo ya kiuchumi. “ NO REFORM NO ELECTION’’ Kampeni hii si njema kwetu kwa tunaotaka heshima na taratibu zetu za kukimbizana na maisha ya kila siku.

Si kila kinachoaminishwa kuwa ni “mapambano ya haki” kina nia njema, hapana ndani ya hayo kuna giza nene na mashimo; tusitumbukie.

Mshikamano Kwanza, Maslahi Binafsi Baadaye

Tushikamaneni, hakuna kitu kisicho na utaratibu. Kama kweli kuna madai ya msingi kuhusu mabadiliko ya kisiasa, wapo wenye nia njema. Pia, kuna njia za kitaratibu, heshima, busara na kisheria za kuyashughulikia badala ya kutumia nguvu na Mihemko kwa ulazima.

Kampeni ya “No Reform, No Election” ni jaribio la kusambaratisha mshikamano wetu na kuzorotesha maendeleo ya uchumi wetu. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, “Binadamu huweza kudanganywa kwa muda, lakini si milele.” Tusikubali kudanganywa na ajenda za wenye nia ovu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here