MGOMBEA wa kiti cha Urais kupitia CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwasili Pemba, Septemba 24, 2025, kwa ajili ya kuzungumza na Wafanyabiashara na Wajasiriamali katika Soko la Chakechake, Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.