Ni wajibu kuandaa jamii yenye maadili na hofu ya Mungu – Rais Mwinyi

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ni wajibu kuandaa jamii yenye maadili na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati wa fainali za Mashindano ya 24 ya Kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Sururu Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam, Machi 9, 2025.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kazi kubwa imefanyika kuwaandaa vijana kuwafundisha kukihifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu (Quran).

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Taasisi ya Aisha Sururu Foundation cha Mafunzo ya Quraan na ufundi stadi katika eneo la Kiparan’ganda , Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Aisha Sururu Foundation kwa kuendelea kuyaandaa mashindano ya Kuhifadhisha Quran hadi ngazi ya Taifa kwa kushirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Vilevile kwa kuweka mazingatio maalum ya kuwasaidia wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupitia Taasisi hiyo.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuziomba Taasisi mbalimbali na watu wenye uwezo kusaidia kufanikisha shughuli za kidini ikiwemo za Kuhifadhisha Quraan ili kuzidi kuuimarisha Uislamu na kupata fadhila nyingi kwa Mwenyezi Mungu.

Washindi mbalimbali wa mashindano hayo ya kuhifadhi juzuu 3, 5, 10, 20 na 30 wamepatiwa zawadi za fedha taslimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here