Ni Dkt. Samia na Dkt. Mwinyi 2025

0

KATIBU wa NEC, Idara ya Oganaizesheni ya Chama, Issa Haji Ussi ‘Gavu,’ amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ndiyo pekee watakaopeperusha bendera katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza wakati alipomwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kufungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, Gavu alisema Rais Dkt. Samia na Rais Dk. Mwinyi wamefanya kazi kubwa na nzuri.

Gavu akizungumza katika mafunzo hayo, yaliyotanguliwa na kongamano la kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 katika miaka mitatu ya uongozi wake lililoandaliwa na UWT.

“Watu wawili hao, viongozi wawili hao, ndiyo turufu na tegemeo la Chama Cha Mapinduzi hivi sasa. Hatuna mgombea mwingine atakayesimama kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ni Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hakuna mgombea mwingine atakayesimama kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa tiketi ya CCM ni Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Katika kongamano hilo, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda alimkabidhi mgeni rasmi hati ya shukrani ya Rais Dkt. Samia kumpongeza na kumshukuru kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kishindo na Silingi Milioni Mbili za kuchukulia fomu ya kuwania kiti hicho wakati utakapowadia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here