Mtoto atolewa ‘Screw’ kwenye mapafu

0

Na Mwandishi Wetu

MTOTO mwingine ametolewa Skrubu (Screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera na kwenda kuinasa na kisha kuitoa ambayo alikua akiichezea kinywani mwake wakati akiwa shuleni na hatimaye kumpalia na kisha kukwama na kushindwa kutoka.

Bingwa wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Mwanaada Kilima alisema, mtoto huyo alipaliwa na skrubu hiyo siku nne zilizopita ambayo iliyoingia kwenye mapafu yake na kusababisha kukohoa sana na kushindwa kutoka kwa njia ya kawaida.

Msafiri Chatanda, mzazi wa mtoto huyo amewashukuru watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa waliyofanya tangu alipofikishwa hospitali hapo na kufanikisha kutoa skurubu hiyo.

Aidha, amewaasa wazazi kuwa watoto wamekuwa na desturi ya kuchezea vitu lakini hakuna mzazi anaangaika kumkumbusha mtoto madhara yake na kuona kuwa ni kitu cha kawaida.

Katikati ya mwezi huu, Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lilifanikiwa kuondoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Mapema jana, Daktari wa Magonjwa ya Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dkt. Hedwiga Swai akishirikiana na wenzake walifanikiwa kumtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto alilodumu nalo kwa miaka 11 kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi lilipo na kulinasa na kisha kulitoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here