MOI tutaendelea kuwahudumia wagonjwa wa NHIF – Prof. Makubi

0
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi.

Na Abdallah Nassoro – MOI

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesema imejiandaa vema kuwapokea wagonjwa wote wakiwemo waliokuwa wanatibiwa hospitali binafsi kutokana na hospitali hizo kusitisha kutoa huduma kwa kutumia Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF).

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Makubi amebainisha hayo wakati alipokuwa anajibu swali la mteja aliyetaka kujua iwapo MOI inaendelea kutoa huduma kwa kutumia Bima ya NHF.

Alisema, Taasisi ya MOI imejiandaa vizuri kuwahudumia wagonjwa hao waliokuwa wakitibiwa hospitali binafsi ambazo wamesitisha huduma za NHIF ikiwa pamoja na kutoa huduma siku za Jumamosi na Jumapili.

“Sisi MOI baada ya kuona hayo matangazo kuwa hospitali binafsi zimesitisha huduma za NHIF, tutaendelea kuwahudumia wagonjwa wa NHIF kama kawaida, hakuna mgonjwa atakayekosa matibabu kutokana na kitita kipya cha NHIF” alisema Prof. Makubi na kuongeza

“Kama itatokea wamekuja MOI kwa kufuata utaratibu uliopo wagonjwa wote watapatiwa matibabu…kwa wagonjwa wa nje tumejipanga kuongeza vyumba vya madaktari na kwa wale wagonjwa wa kulazwa tumejipanga kuongeza vyumba vya kulaza…

Kitengo chetu cha dharura tumekiongezea wataalam ili kukidhi mahitaji ya wakati husika sanjari na vyumba vya operesheni… tumejipanga kutoa huduma siku za wikiendi, hata kama atakuja mwananchi anahitaji operesheni watumishi watakuwa hapa kuendelea kutoa huduma”

Alisisitiza kuwa, hata kama wagonjwa wataongezeka MOI imejipanga kutoa huduma, na kwamba wataongeza huduma kwa siku mwisho wa wiki jumamosi na jumapili watumishi

Pro. Makubi alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya ndugu wa mgonjwa Christina Saligwe kuuliza iwapo Taasisi ya MOI itaendelea kutoa huduma kutumia kadi za NHIF au laa.

Aidha, aliridhia ombi la ndugu wa wagonjwa la kutaka kuwepo kwa viti pembeni mwa kitanda cha mgonjwa ili muuguzi akitumie kwa ajili ya kukaa.

“Tumeagiza viti zaidi ya 300 ili tuweze kuweka wodini kwa ajili ya waguzi na nfugu kukaa wanapokwenda kuwaona wagonjwa, hii ni hospitali yenu na ni lazima tuiboreshe” alisema Prof. Makubi.

Taasisi ya MOI imejiwekea utaratibu wa kusikiliza maoni kutoka kwa wateja wake kila siku ya Jumatano na Ijumaa kwa lengo la kuboresha huduma zake kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here