Minara 652 yakamilika na kuanza kutumika

0

SERIKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa jumla ya minara 758 ya mawasiliano vijijiini.

Hadi sasa, minara 652 imekamilika na tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi, hatua inayopanua wigo wa upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini.

Minara hiyo imewezesha kufikishwa kwa huduma ya mawasiliano ya simu katika maeneo ambayo awali yalikuwa na changamoto kubwa ya mawasiliano, hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here