Minara 602 kati ya 758 ya mawasiliano vijijini, imewaka na imeanza kutoa huduma

0

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini.

Hadi sasa, jumla ya minara 602 kati ya 758 iliyopangwa kujengwa imekamilika na tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi. Hii ikiwa ni sawa na asilimia 79.42 ya utekelezaji wa mradi huo.

Kupitia utekelezaji huu, Serikali inalenga kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata huduma bora na za uhakika za mawasiliano, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha usawa wa upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa Watanzania wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here