Mbeto afichua jinsi OMO alivyokataliwa Pemba

0

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

KATIBU wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi – Zanzibar Khamis Mbeto Khamis amesema, mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othman (OMO) ana wakati mgumu na anakataliwa kila anapokwenda.

Mbeto alisema, hivi karibuni OMO alijaribu kumuiga mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Hussein Mwinyi kukutana na masheikh, matokeo yake wakamtakaa.

Alisema, masheikh hao walimuweka wazi kwamba, kama anataka kupata mafanikio na iwapo anataka Zanzibar iendelee kupata maendeleo, afuate nyayo za Dkt. Mwinyi ambaye amehakikisha kwa kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane, kuna amani, utulivu na umoja.

Mbeto alisema, mbali na Masheikh hao, OMO alikwenda Kiwani, wananchi wakakataa kumkaribisha kwenye nyumba zao na akazomewa, akakimbilia Kengeja, Jimbo la Mtambile ambako nako mambo yalikuwa magumu kwake.

Mwenezi huyo alisema, mgombea pekee ambaye anakubalika na makundi yote na kila anapopita ni Dkt. Hussein Mwinyi, hivyo kwenye uchaguzi ujao hana upinzani na ana uhakika wa kupata kura za kishindo kutokana na maendeleo aliyoyafanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here