Manyara na Mwanza mabingwa riadha Mita 800

0

CATARINA Charles kutoka Mkoa wa Mwanza na Joshua Gidawaghaida wa Manyara, wameibuka washindi katika fainali ya riadha Mita 800 Wasichana na Wavulana, katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi na Sekondari.

Fainali hiyo imefanyika asubuhi ya Juni 14, 2025, katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Kleruu Manispaa ya Iringa ambapo Catarina aliyeibuka mshindi wa mita 800 kwa Wasichana alitumia dakika 2:30:22 na kwa wavulana Joshua alitumia dakika 2:11:7.

Naye Joyce Maganga aliuwakilisha vema Mkoa wa Mara kwa kushika nafasi ya pili akitumia dakika 2:32:13, na Mariam Gadiye wa Manyara akashika nafasi ya tatu akitumia dakika 2:33:27.

Upande wa Wavulana Isack Michael wa Kilimanjaro alishika nafasi ya pili kwa kukimbia dakika 2:14:63 na Manyara ikashika nafasi ya tatu baada ya Apolinary P Apolinary kukimbia kwa dakika 2:15:91.

Mchezo wa riadha uko katika hatua mbalimbali kwenye UMITASHUMTA 2025, ambapo licha ya fainali ya Mita 800, pia kumefanyika nusu fainali ya Mita 400 kupokezana vijiti, mita 1,500, fainali ya mita 200 na fainali ya kuruka yote ikiwa ni kwa wasichana na wavulana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here