Makalla: Chadema mnavuna mlichopanda

0

• Asema viongozi wamekiua chama chao kwa mikono yao wenyewe

• Wamepoteza ndoto za wagombea udiwani na ubunge

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema watu wanaondoka katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa sababu wamekosa matumaini.

Makalla ameeleza hayo leo Aprili 9 wakati akizungumza na wananchi katika Kata ya Lupiro kwenye mkutani uliojumuisha wananchi wa Wilaya mbili ya Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro, katika mfululizo wa ziara yake mkoani humo.

Makalla alisema, katika chama hicho kulikuwa na watu wenye ndoto na matamanio ya kugombea udiwani, ubunge na viti maalumu, lakini matumaini hayo yamefifishwa, ndio maana wameondoka na si kufanya usaliti.

“Anawatuhumu wenzake kwamba wamewasaliti sio wamewasaliti wamekosa matumaini kulikuwa na watu walikuwa wanataka udiwani, ubunge na urais lakini uongozi wa sasa umeondosha matumaini hayo,” alisema Makalla.

Aliongeza kwa kuwataka waache kunyoosheana vidole kwa kuambiana kuwa wanaoondoka wamekuwa wasiliti, kwani kinachotokea ni matokeo ya mpasuko walioutengeneza ndani ya chama na kufanya wapoteze muelekeo na mvuto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here