MAFUNZO ya mfumo wa Kieletroniki wa ukaguzi na ufuatiliaji(IFT-MIS) yamefanyika Leo 04 ,Machi 2025 katika Halmashauri ya wilaya ya Kibaha.
Mafunzo hayo yametolewa kwa wakuu wa Idara na vitengo ndani ya halmashauri ili yaweze kuwasaidia katika kujibu hoja zitakazo tumwa ndani ya mfumo wa ukaguzi.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Afisa Tehama Menard Mvimbile amewataka wakuu wa Idara na vitengo kuzingatia kuzingatia mafunzo waliyopata kwani itawasaidia kuelewa na kutumia mfumo kwa urahisi.
Afisa Tehama alihitimisha kwa kusisitiza kua Mafunzo hayo yatakua endelevu hivyo watumishi wanapaswa kuhudhuria Mafunzo yote yatakayo pangwa kwa Muda husika.