Korea Kaskazini wazua balaa Japan

0
North Korean leader Kim Jong Un speaks during the Third Enlarged Meeting of the Seventh Central Military Commission (CMC) of the Workers' Party of Korea (WPK) in this undated photo released on December 22, 2019 by North Korea's Korean Central News Agency (KCNA). KCNA via REUTERS ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. REUTERS IS UNABLE TO INDEPENDENTLY VERIFY THIS IMAGE. NO THIRD PARTY SALES. SOUTH KOREA OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN SOUTH KOREA.

Pyongyang

KOREA Kaskazini imefyatua kombora lake la ‘balestiki’ kuelekea upande wa Japan, na kusababisha kusitishwa kwa usafiri wa treni katika baadhi ya maeneo, huku Wajapani katika maeneo ya Kaskazini wakitakiwa kujificha.

Majeshi ya Japan na Korea Kusini yamethibitisha kwa nyakati tofauti hatua ya Pyongyang kuvurumisha kombora lake hilo la masafa ya kati (IRBM), lililopaa katika anga ya maeneo ya Kaskazini mwa Japan.

Mkuu wa Majeshi ya Japan akinukuliwa na PARS alisema, kombora hilo limefyatuliwa kutoka mkoa wa Jagang wa Korea Kaskazini, na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Pyongyang kufanya hivyo tokea mwaka 2017.

Serikali ya Tokyo imesema, kombora hilo la Korea Kaskazini limedondoka katika Bahari ya Pacific, baada ya kupita katika anga ya Japan. Inaarifiwa kuwa, liliruka zaidi ya Kilomita 4,500 katika anga ya Japan, na umbali wa Kilomita 970 juu ya usawa wa bahari.

Msemaji wa serikali ya Tokyo, Hirokazu Matsuno alisema, Msururu wa vitendo vya Korea Kaskazini yakiwemo majaribio ya makombora yake ya balestiki, unatishia amani na usalama wa Japan, na kwa jamii yote ya Kimataifa.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amelaani kitendo hicho, huku Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol akionya kuwa nchi hiyo itatoa jibu mwafaka kwa uchokozi huo wa Pyongyang.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, Korea Kaskazini imefanya majaribio zaidi ya 20 ya silaha zake huku sehemu kubwa ya majaribio hayo ikiwa ni kufyatua makombora yake ya balestiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here