Kishindo cha Dkt. Mwinyi, uzinduzi wa kampeni Pemba

0

MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Unguja leo Jumatatu, Septemba 15, 2025 na kuwasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya Uzinduzi wa Kampeni za CCM.

Dkt. Mwinyi amewasili katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, ambako ndiko kumeandaliwa uzinduzi rasmi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Pemba.

Uzinduzi huu unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, viongozi wa Chama na Serikali, pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii, huku Dkt. Mwinyi akitarajiwa kueleza dira na vipaumbele vya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here