Kibaha yajipanga kuboresha lishe kwa wanafunzi na wajawazito

0

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon, amewataka Maafisa Elimu na Watendaji wa Kata kushirikiana kuanzisha bustani za matunda mashuleni ili kusaidia wanafunzi kupata mlo kamili, kama ilivyofanikiwa kwa bustani za mboga.

Akizungumza Mei 29, 2025 katika kikao cha Kamati ya Lishe kilichofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Nickson pia aliagiza elimu ya lishe kuendelea kutolewa kwa wajawazito ili kupunguza tatizo la upungufu wa damu (anemia).

Afisa Lishe wa Halmashauri, Coletha Chapile, alisema kiwango cha udumavu kwa watoto kimepungua sana watoto chini ya miaka mitano

Pia, alieleza kuwa asilimia ya wanafunzi wanaopata mlo angalau mmoja shuleni imeongezeka kutoka 98.4 hadi 98.9.

Hata hivyo, alitaja changamoto ya wajawazito kuchelewa kuanza kliniki, ambapo asilimia 24 ya walioanza hudhurio walikuwa na ujauzito zaidi ya wiki 12 – hali inayochangia ongezeko la anemia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here